Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 18 June 2013

Vikosi vya usalama vya Misri vyajiweka tayari

                                  
Duru za usalama za Misri zimetangaza kuwa vikosi vya jeshi la nchi hiyo vimejiandaa kulinda hali ya usalama wakati wa kufanyika maandamano ya tarehe 30 mwezi huu.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri pia imeziagiza idara zote za usalama na nyinginezo kuwa tayari kulinda usalama wa taasisi mbalimbali za nchi, balozi na idara za serikali huko Cairo mji mkuu wa Misri na katika mikoa mingine ya nchi hiyo.
Makundi ya kisiasa yanayompinga Rais Muhammad Morsi wa Misri wametaka kufanyika maandamano makubwa tarehe 30 mwezi huu wa Juni sambamba na kutimia mwaka mmoja wa kuweko madarakani rais huyo.
Wapinzani wa Morsi wanataka kufanyika maandamano hayo ili wamtake Morsi ajiuzulu madarakani na kufanyike uchaguzi wa Rais wa Misri kabla ya wakati.  

 

0 comments:

Post a Comment