Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 18 June 2013

Iran yaingia Kombe la Dunia Brazil 2014

                       
  Timu ya Taifa ya Soka ya Jamhuri ya Iran leo imeifunga Korea Kusini bao moja kwa nunge na hivyo kufanikiwa kupata tiketi ya kushiriki katika Fainali  za KombAe la Dunia nchini Brazil mwakani.
Katika mechi hiyo ngumu sana iliyochezwa leo usiku kwa wakati wa Korea Kusini katika uwanja wa Ulsan Munsu mjini Seoul, bao la ushindi la Iran lilipachikwa wavuni na mshambuliaji shupavu Reza Ghoochan-Nejad katika dakika ya 59 na kuiwezesha Iran kuongoza  kundi A la Asia ikiwa na pointi 16. Korea Kusini imemaliza ya pili kwa pointi 14 na kufuzu pia kuingia Kombe la Dunia kutokana na wingi wa mabao ya kufunga licha ya kuwa ia pointi sawa na Uzbekistan ambayo nayo imeifunga Qatar 5-1 huko Taskent. Korea Kusini imefuzu kuingia Kombe la Dunia kwa mara ya tisa huku Iran ikishiriki kwa mara ya nne ambapo mara ya mwisho ilishiriki mwaka 2006.
Sherehe zimetanda kote Iran baada ya ushindi huo huku maelfu wa wananchi wakimiminika katika mitaa ya Tehran. Timu ya Taifa ya Iran inatazamiwa kukaribishwa kwa taadhima wakati itakaporejea hapa Tehran kutoka Korea Kusini.

0 comments:

Post a Comment