
Umati
mkubwa wa waumini walimiminika kutaka kusikia mawaidha yake kwa mara ya
kwanza baada ya kutoka gerezani juzi. Katika tukio hilo, waumini pia
walichanga fedha kwa ajili kumwezesha Sheikh Ponda kugharimia matibabu
ya afya yake na sehemu ya fedha hizo walipewa mawakili wake ili wafanye
maandalizi ya kukata rufaa.
Pia Mei 18 mwaka huu, waumini hao
wamepanga kufanya dua (Itikafu) itakayofanyika katika msikiti wa
mtambani kwa ajili ya kumwombea Sheikh Ponda na wenzake.
ust
Mukadam alimshukuru Allah kwa kuwapa adhabu ya ugonjwa,watu kadhaa
akiwemo 'mkubwa mmoja' alie mahu2ti sauz afrika(alihusika kuwatengenezea
mashtaka),na afisa mwingne wa jesh kufarik ajalini baada ya
kuwanyanyasa selo! Pia mkubwa mmoja wa jesh ambae ni msabato kuwatamkia
kua 'waislamu mnaonewa' mara baada ya kuwahoji. Akamaliza kwa kusema 'ni
wakati wa waislamu kujipanga' nae SHEIKH PONDA. alisema
'nitapambana hadi mwisho' huku watu wakisema takbir alah akbar! Amesema
Wakristo wanapendelewa na serikali. Serikali ilisema aliekojolea kuran
ni mtoto,wakati ye kawakuta watoto jela! Akiwemo wa miaka 10,aliyekwapua
mkoba.,ila yule mkristo wa miaka 14 serikali ilisema mtoto na
haikumchukulia hatua zozote!
“Wamekuwa wakinitungia njama za
kuniondoa kwa misingi ya kuwa mimi siyo Mtanzania, hakuna wa kuniondoa
hapa nchini na nitapambana hadi hatua ya mwisho na kuhakikisha kuwa
Waislamu wanapata uhuru wao,” alinena Sheikh Ponda.
Pia kasema
anazo cd,zikionyesha jins serikali inavoua na kupanga kukandamiza
uislamu.pia Kampongeza sana Zitto kabwe kwa mchango wake wa kutetea
uislamu bungeni na kamponda yule aliepeleka cd alizoita za uchochezi
bungeni! Karudia kusisitiza kuwa NECTA kuna udini na Waislamu
wanafelishwa! na pia serikali inapendelea na kuendeshwa na wakristo. Pia
alihoji kuhusu bomu la Arusha kuwa, wamekamatwa waarabu ,mbona
hawajakamata wazungu? Anasema huo ni mpango wa kuonea waarabu na
uislamu!
Pia kasema wakristo hawajawahi kuuwawa na serikali,ila
waislamu tu ndo wanauawa! Mwembechai waliuawa, Pemba waliuawa. na hata
Pemba Waislamu waliuawa na serikali iki2mwa na Kanisa! amesema pemba
kuna helcopter zilikua zinalipua majahazi ya waislamu(wakiwa baharini)
wakati wanakimbilia Mombasa na Tanga.!
Pia kasema,nchi hii hakuna
udini,ila kuna mapambano ya waislamu kudai haki zao na redio iman
imefungiwa kuwaonea waislamu wasipate pa kusemea(ile ya wakristo haikua
lengwa)!Kwa kifupi shekh kaapa atapambana kwa nguvu kubwa.
pia
alihudhuria Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alielezea
kusikitishwa kwake juu ya kauli kwamba Sheikh Ponda asingeweza kupata
dhamana katika kesi iliyokuwa ikimkabili.
“Vyombo vyetu haviko
makini, tuliambiwa Ponda hawezi kupata dhamana lakini leo hii amefungwa
kifungo cha nje, hii inatia shaka na uamuzi uliokuwa ukiendelea,”
alisema Profesa Lipumba.
0 comments:
Post a Comment