Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 13 June 2013

Uturuki kuitisha kura ya maoni kuhusu bustani ya Gezi



 Serikali ya Uturuki imesema kuwa huenda ikaitisha kura ya maoni kuhusiana na mpango wa kubomolewa bustani ya Gezi iliyoko karibu na meidani ya Taksim mjini Istanbul ili kujaribu kumaliza maandamano ya kupinga serikali yanayoendelea nchini humo.
Huseyin Celik, msemaji wa chama tawala cha AKP amesema hayo baada ya mazungumzo yaliyofanyika kati ya Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan na baadhi ya wawakilishi wa wandamanaji mjini Anakara. Celik amesema, suala hilo litaamuliwa kwa kura ya maoni ili uamuzi utakaochukuliwa umalize maandamano na mikusanyiko kwenye bustani hiyo.
Hayo yanajiri huku waandamanaji wakiendelea kujikusanya kwenye meidani ya Taksim karibu na bustani ya Gezi na kuendelea kupambana na polisi wanaotumia nguvu kuwatawanya. Jeshi la polisi nchini Uturuki limetuhumiwa kutumia nguvu za ziada kuwatawanya waandamanaji.
Machafuko nchini Uturuki yalianza Mei 31 baada ya polisi kuwatawanya wandamanaji kwa maji na gesi za kutoa machozi wakati waandamanaji hao walipokuwa wanapinga kubolewa bustani hiyo ambayo ni eneo muhimu la makutano ya watu mjini Istanbul.

0 comments:

Post a Comment