Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 13 June 2013

AU yazitaka Misri na Ethiopia kufanya mazungumzo




Umoja wa Afrika umezitaka Misri na Ethiopia kutatua hitilafu zao kwa njia ya mazungumzo kuhusiana na ujenzi wa bwawa la an Nahdha la Ethiopia katika Mto Nile.
Matamshi hao yalitolewa jana na Nkosazana Dlamin-Zuma, Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, baada ya Rais Muhammad Mursi wa Misri kusema kwamba nchi yake inaweza kuchukua hatua zozote hata za kijeshi ili kuzuia ujenzi wa bwawa hilo la Ethiopia.
Zuma sambamba na kuashiria kwamba Misri na Ethiopia zote zinahitajia maji ya Mto Nile amesisitizia ulazima wa nchi hizo kutafuta njia za kiusalama za kutatua mgogoro huo.
Misri inasema kuwa, haki yake ya kustafidi na maji ya Mto Nile inalindwa na mikataba miwili ya mwaka 1929 na 1959 na kwamba hatua ya Ethiopia ya kujenga bwawa hilo inapunguza kiwango kikubwa cha fungu la Cairo la maji  hayo.
Hata hivyo Ethiopia nayo inasema haitokubali kusimamisha mradi wake huo wa kujenga bwawa ili kuzalisha umeme kwani ni haki yake kutumia rasilimiali zake yakiwemo maji.



0 comments:

Post a Comment