Wagombea wa uchaguzi wa rais nchini Iran wamemaliza rasmi kampeni zao
leo saa mbili asubuhi. Akihutubia katika mji wa Birjand kusini mwa nchi,
Ali Akbar Velayati alisema, baraza la mawaziri linapaswa kuwa la
wataalamu na kwamba wanapaswa kusaidia vijana wenye vipaji kuendeleza
nchi. Mgombea Saed Jalili amefunga kampeni zake za uchaguzi huko mkoani
Golestan ambapo amewaambia wafuasi wake kuwa, Iran ina uwezo wa kutatua
matatizo yake ya ndani kama vile ughali wa maisha na ukosefu wa ajira,
kama ilivyoweza kusimama kidete dhidi ya maadui. Mohsen Rezai ameeleza
katika mahojiano na waandidhi habari kwamba, sera zake yeye ni
kutoonyesha msimamo mkali iwapo Wamagharibi watataka kulegeza misimamo
yao na kwamba ni bora Wamagharibi waondoe vikwazo ili kuimarisha
uhusiano wa kibiashara wa pande mbili na kuimarisha uchumi wao. Naye
Mohammad Gharazi amesema, kila mkoa unapaswa kuendesha mambo yake
wenyewe na baadaye kuripoti kwa serikali kuu. Mgombea Muhammad Qalibaf
alihitimisha kampeni zake mjini Isfahani ambako alitoa wito kwa wananchi
wajitokeze kwa wingi kupiga kura na kuahidi kuleta maendeleo makubwa ya
kiuchumi iwapo atachaguliwa. Hii ni katika hali ambayo Hassan Rohani
ameahidi kuimarisha uhusiano na nchi za dunia, akisema kwamba serikali
yake itayapa kipaumbele matatizo ya uchumi. Uchaguzi wa rais wa Iran
utafanyika kesho Ijumaa, Juni 14.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment