Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 4 June 2013

Somalia yahofia usalama wa raia wake Afrika KusiniSerikali ya Somalia imeitaka serikali ya Afrika Kusini kulinda maisha ya raia wa nchi hiyo walioko nchini humo. Waziri Mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon amemtaka Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini kuchukua hatua madhubuti za kukomesha mashambulizi yanayofanywa dhidi ya raia wa kigeni wakiwemo Wasomali nchini humo. Wiki iliyopita baadhi ya maeneo yaliyoko pambizoni mwa miji ya Johannesburg na Port Elizabeth huko Afrika Kusini yalishuhudia mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya wafanyabiashara na wachuuzi wa Kisomali walioko nchini humo. Kwenye shambulio lililofanyika karibu na Port Elizabeth raia mmoja wa Somalia aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.


0 comments:

Post a Comment