Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 4 June 2013

Bunge la Sudan laliunga mkono jeshi la nchi hiyo




 Bunge la Sudan limesisitiza juu ya ulazima wa kuungwa mkono jeshi la nchi hiyo katika kuwaangamiza waasi katika maeneo mbalimbali nchini humo. Mehdi Ibrahim Mkuu wa Mrengo wa 'Kongresi ya Taifa' katika bunge la Sudan amesema kuwa, uungaji mkono kwa jeshi la nchi hiyo katika kuwasambaratisha waasi, ni jukumu la kitaifa. Ameongeza kuwa, operesheni za kuyakomboa maeneo yaliyokuwa yakidhibitiwa na makundi ya waasi katika jimbo la Kordofan Kusini zinapasa kuendelea na kuwataka wananchi waliunge mkono jeshi la nchi hiyo. Mbunge huyo kutoka mrengo wa Kongresi ya Taifa amesisitiza juu ya kuongezwa bajeti ya jeshi, kwa lengo la kununua zana na silaha za kisasa na kuboresha hali ya kimaisha ya wanajeshi wa nchi hiyo. Serikali ya Sudan imekuwa ikizituhumu nchi za Sudan Kusini, Uganda na utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa zinayaunga mkono makundi ya waasi katika maeneo ya kusini na magharibi mwa Sudan.

0 comments:

Post a Comment