Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 25 June 2013

Rais Rousseff wa Brazil kuitisha kura ya maoni


Rais Dilma Rousseff wa Brazil ameelezea uamuzi wa serikali ya nchi hiyo wa kuitisha kura ya maoni juu ya marekebisho ya kisiasa nchini humo.
Rais Rousseff amesema kuwa, serikali ya Brazil imeamua kuitisha kura hiyo ya maoni kwa shabaha ya kukomesha maandamano dhidi ya serikali na machafuko ya kijamii yaliyoikumba nchi hiyo.
Mara baada ya kufanya mazungumzo na magavana, mawaziri na mameya wa miji yote nchini humo, Rais Rousseff ameongeza kuwa, suala la kufanyika marekebisho ya kisiasa limekuwa likipewa kipaumbele na serikali na kusisitiza kuwa, hivi karibuni watachaguliwa  wajumbe wa jopo litakalokuwa na jukumu la kutayarisha mchakato wa mabadiliko ya kisiasa nchini humo.
Wananchi wa Brazil wamekuwa wakiandamana wakipinga gharama kubwa za kuandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2014 nchini humo, wa kunataka kwanza iboreshwe hali ya maisha na huduma za umma kwa wananchi

0 comments:

Post a Comment