Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 25 June 2013

Meja Jenerali al Graidy aituhumu serikali ya Libya
 


Mkuu wa vikosi vya majeshi ya Libya ameituhumu baadhi ya mirengo iliyoko kwenye bunge la nchi hiyo kwa kufanya njama za kuzorotesha mwenendo wa kulijenga upya jeshi la nchi hiyo.
Akizungumza kwenye ukumbi  wa bunge la Libya, Meja Jenerali Salim al Gnaidy ameituhumu pia serikali ya Tripoli kwa kuingilia masuala ya jeshi na kutoa amri na maamuzi ya kijeshi bila ya kufanya mawasiliano yoyote na viongozi wa ngazi za juu wa jeshi. Meja Jenerali al Gnaidy ameongeza kuwa, kuna ulazima wa kutengwa bajeti ya kutosha kwa lengo la kulikarabati jeshi la nchi hiyo na ameikosoa mirengo inayofanya njama za kutaka bajeti ya jeshi ipunguzwe.
Baada ya kuangushwa utawala wa Kanali Muammar Gaddafi, kiongozi wa zamani wa Libya, serikali ya nchi hiyo imekuwa ikifanya juhudi za kulijenga upya jeshi la nchi hiyo na kulipatia zana na silaha za kisasa.

0 comments:

Post a Comment