Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 25 June 2013

Hollande kupambana na chuki dhidi ya Uislamu


Rais Francois Hollande wa Ufaransa ameahidi kupambana na vitendo vya uadui na chuki dhidi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu nchini humo. Akizungumza mbele ya mjumuiko mkubwa wa wawakilishi wa taasisi na asasi za kiserikali na kiraia pambizoni mwa Paris, Rais Hollande amesisitiza kuwa, vitendo vya chuki na ubaguzi hasa dhidi ya Waislamu vinapaswa kukomeshwa. Miongoni mwa vitendo vya chuki na uadui dhidi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu mwaka huu, ni mashambulizi kadhaa yaliyofanywa dhidi ya wanawake waliovaa hijabu ya Kiislamu katika eneo la Val- d'Oise kaskazini mwa Ufaransa. Viongozi wa Muungano wa Taasisi za Kiislamu nchini Ufaransa UOIF wamesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba, chuki na uadui dhidi ya Waislamu limekuwa jambo la kawaida nchini humo na wamewataka viongozi wa serikali ya Paris kuvunja kimya chao na badala yake kukabiliana na vitendo hivyo viovu.
Nalo Baraza la Utamaduni la Waislamu nchini Ufaransa CFCM limetangaza kuwa, zaidi ya Misikiti 10 imeshavunjiwa heshima tokea kuanza mwaka huu wa 2013.

 

0 comments:

Post a Comment