Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 25 June 2013

Misri yazipiga marufuku ndege za Israel
Waziri wa Huduma za Anga za Misri Wael al Maadawi amesisitiza kuwa, ndege zote za utawala wa Kizayuni wa Israel ambazo zitakuwa na mfumo wa makombora, hazitaruhusiwa kutua kwenye viwanja vya ndege au kupita kwenye anga ya nchi hiyo.
Al Maadawi amesema kuwa, hatua hiyo imechukuliwa baada ya shirika la ndege la utawala wa Kizayuni wa Israel kudai hivi karibuni kwamba limeamua kuweka mfumo wa kujilinda na makombora kwenye ndege zake zote za abiria ili kulinda maisha na usalama wa abiria katika kukabiliana na mashambulio ya kigaidi.


0 comments:

Post a Comment