Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 20 June 2013

Mwanamke Mwislamu mjamzito ahujumiwa Ufaransa

Katika siku za hivi karibuni nchini Ufaransa kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la hujuma dhidi ya wanawake Waislamu wanaovaa hijabu, mitandio au burka.
Hiyo juzi mwanamke Mwislamu aliyekuwa amevaa Hijabu alishambuliwa na magenge ya kibaguzi ya Wanazi mamboleo katika kitongoji cha Paris cha Argenteuil. Imearifiwa kuwa mwanamke huyo aliye na umri wa miaka 21 alikuwa na mimba ya miezi minne ambayo aliipoteza kufuatia hujuma hiyo. Wakili wake anasema alishambuliwa barabarani na watu ambao walijaribu kupasua mtandio wake huku wakimpiga mateke tumboni.
Kufuatia kitendo hicho cha kinyama, watu waliokuwa na hasira waliandamana mbele ya ofisi za meya wa Argenteuil kulalamikia ongezeko la hujuma za magenge ya Wanazi mambo-leo dhidi ya Waislamu. Meya wa mji huo amelaani hujuma hiyo na kusema hatakubali chuki kutekelezwa dhidi ya Uislamu au Islamophobia katika mji huo. Hata hivyo Waislamu wanasema makundi ya Wanazi mamboleo vipara yameonekana mjini humo na kwamba hakuna hatua zozote za kisheria zinazochukuliwa dhidi yao.

0 comments:

Post a Comment