Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 20 June 2013

Masaibu ya Wapalestina waliozingirwa na Israel

Mzingiro wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza unaingia mwaka wake wa sita katika mwezi huu wa Juni ambapo maelfu ya Wapalestina wanaendelea kukumbwa na masaibu ikiwa ni pamoja na kukosa haki za msingi za binaadamu.
Gaza imekuwa chini ya mzingiro wa utawala haramu wa Israel kutoka mwezi Juni mwaka 2007. Mzingiro huo wa kinyama umepelekea hali ya maisha kuzorota kwa sababu Israel imewazuia wakaazi wa Ghaza haki ya kununua vyakula, dawa na vifaa vya ujenzi. Jo Harisson wa shirika la kutoa misaada ya Okfam anasema asilimia 80 ya Wapalestina huko Ghaza wanaishi kwa kutegemea misaada. Mtetezi wa haki za binaadmau kutoka Uingereza Adie Mormech anasema jamii ya kimataifa haijachukua hatua zozote kusitisha mzingiro wa Israel dhidi ya Wapalestina huko Ghaza. Anasema Ghaza ina idadi ya watu milioni 1.7 ambapo nusu yao ni watoto. Mtetezi huyo wa haki za binaadmau anasema kuwaadhibu watu wa Ghaza ni jambo ambalo linakiuka sheria za kimataifa. Israel iliweka mzingiro wa ardhi, anga na baharini dhidi ya watu wa Ghaza baada ya hatua yao ya kuichagua serikali ya Harakati ya Kiislamu ya Palestina Hamas katika uchaguzi wa kidemokrasia

0 comments:

Post a Comment