Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 20 June 2013

Machafuko yaendelea Misri
Watu wasiopungua 27 wamejeruhiwa katika mapigano baina ya wafuasi na wapinzani wa rais Mohammad Morsi wa Misri.
Machafuko hayo ya Jumatano katika mkoa wa Fayoum yaliibuka baada ya mkutano ulioitishwa na harakati ya Ikwanul Muslimin kumuunga mkono Rais Morsi.
Machafuko yaliibuka pia katika eneo la Nile Delta baada ya rais Morsi kuwateua wanachama kadhaa wa harakati ya Ikanul Muslimin katika nyadhifa muhimu serikalini. Hivi karibuni Rais Morsi aliwateua magavana wapya ambao wote ni wanachama wa Ikanul Muslimin. Hii inamaanisha kuwa magavana 11 kati ya 27 kote Misri ni wanachama wa Ikawanul Muslimin.
Weledi wa mambo wanasema Misri inakabiliwa na hitilafu kubwa za kimitazamo na mgawanyiko wa kijamii na kwamba iwapo masuala hayo mawili hayatotatuliwa haraka, yanaweza kuwaletea madhara Wamisri wenyewe.      


0 comments:

Post a Comment