Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 20 June 2013

Dk. Bilal: Uwezo wa TPA kuhudumia mizigo umeongezeka




Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, amesema uwezo wa Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) kuhudumia mizigo umeongezeka kwa wastani wa asilimia 11.7 , kutoka mwaka 2008 hadi 2012 kwa tani milioni 8.4 hadi kufikia tani milioni 13.1

Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa  mawakala wa ushuru wa forodha katika nchi za Afrika na Mashariki ya Kati uliowakilishwa na wajumbe wanachama kutoka nchi 10 kutoka nchi mbalimbali.

Alisema  ufanisi wa biashara nchini umeongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka tani milioni 11.9 kwa mwaka 2009 hadi kufikia tani 13 kwa mwaka 2012.

Alisema mafanikio hayo yametokana na ufanisi na utendaji wa hali ya juu baina ya ushirikiano wa serikali na sekta binafsi hususani Wizara ya Uchukuzi.

“Mamlaka ya bandari Tanzania inahudumia nchi jirani za Kongo (DRC), Malawi, Zambia,Burundi, Rwanda na Uganda. Kwa nchi ya Kongo wastani wa asilimia 66 wa mizigo husafirishwa, likiwa ni ongezeko la asilimia 17 kwa mwaka 2007,” alisema Dk. Bilal.

0 comments:

Post a Comment