Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 20 June 2013

Daladala zilizoishiwa leseni kurejea katikati ya Jiji Dar


amlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imeanza kutoa leseni kwa  daladala zinazoingia kati kati ya jiji baada ya kusitisha zoezi hilo kwa muda wa mwaka mmoja.


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja Mawasiliano wa Sumtra, David Mziray, alitaja baadhi ya barabara amabzo daladala leseni zake zilisitishwa ni pamoja na ile ya Ali Hassan Mwinyi na Morogoro.


Mziray alisema leseni za daladala hizo zilisitishwa kutokana na kuwapo mpango wa kutoa huduma za usafiri kwa kutumia makampuni.


Hata hivyo, alisema mchakato wa kutangaza tenda ili kupata makampuni umechukua muda mrefu kutokana na taratibu za kisheria hatua ambayo imewafanya waanze kutoa leseni ili huduma hiyo kuendelea kutolewa.


Alikiri kwamba baada ya kusitisha utoaji wa leseni ulijitokeza uhaba wa magari hususani wakati wa asubuhi na jioni na kwamba hivi sasa wafanyabiashara wanaotaka kuingia biashara ya usafirisha wanakaribishwa kuomba leseni.


“Kunzia sasa watu wote wanaotaka kufanya biashara ya daladala wanakaribishwa kuomba leseni mpya kwa kuwa sasa Sumatra imeanza kuzitoa,” alisema.


Hata hivyo, Mziray alisema hana takwimu sahihi ni magari mangapi yaliyositisha kutoa huduma katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya Sumatra kusitisha kutoa leseni.


Akizungungumzia hali halisi ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam, Mziray alisema matengenezo ya barabara za Morogoro na Ali Hassan Mwinyi umechangia kuwapo kwa foleni.


Alisema Sumatra inaweka mikakati ya kukabiliana na daladala zinazokatisha safari zake na kwamba adhabu kali zitatolewa kwa wahusika.


Kuhusu mchakato wa kupata makampuni ya kutoa huduma ya usafiri kwa pamoja, alisema unaendelea vizuri na kwamba lengo la Sumatra na wadau wengine ni kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linakuwa na usafiri wa kuaminika muda wote.
 

0 comments:

Post a Comment