Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 13 June 2013

Bilal aagana na Balozi wa Ujerumani




 Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, amemsifu Balozi wa Ujerumani nchini, Klaus Peter Blandes, kwa kuendelea kuhamasisha mahusiano mema kati ya nchi hizo mbili.

Dk. Bilal alisema hayo jijini Dar es Salaam jana, wakati Balozi Nlandes alipofika ofisini kwake kuagana naye baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.

Balozi Blandes alimueleza Makamu wa Rais kuwa, katika kipindi chake kama Balozi nchini Tanzania, Ujerumani imeendelea kuwa mshirika mzuri wa Tanzania na kwamba ana amini alikuwa anaendeleza historia ya mahusiano mema ambayo yamekuwapo kwa miaka mingi.

Alisema maeneo ambayo Ujerumani imewekeza nchini ni katika sekta za nishati ya umeme na usafirishaji na kueleza kuwa tayari kampuni kadhaa ya nchi hiyo zimeonyesha nia ya kuwekeza katika reli ya kati kwa lengo la kufungua soko kwa nchi za Afrika Mashariki.

Alisema pia Ujerumani ina uwekezaji mkubwa katika sekta ya ujenzi hususani viwanda vya saruji.

Kwa upande wake, Dk. Bilal alisema katika kipindi ambacho Balozi Blandes amekuwapo nchini, uhusiano wa Ujerumani na Tanzania umezidi kuimarika na mchango wa nchi hiyo katika shughuli mbalimbali za maendeleo nchini umekuwa mkubwa.

0 comments:

Post a Comment