Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Monday 10 June 2013

ASAS DAIRIES YAIBUKA KINARA MAONYESHO YA WEEK YA MAZIWA SONGEA 2013

                                

                              01 Shaaban,1434 Hijiriyah/ June10 ,2013 Miyladiyah
 ASAS Dairies imeibuka kinara katika maonyesho ya wiki ya kunywa maziwa kitaifa yaliyo fanyika Songea mwaka huu ambayo yanaandaliwa na Tanzani dairies board (TDB) kwapamoja na Tanzania milk Processor (TAMPA).

Kampuni inayo jihusisha na usindikaji wa bidhaa za maziwa ya ASAS DAIRIES imeibuka mbabe kwa kuwa mshindi wa jumla wa wasindikaji wa bidhaa za maziwa nnchi. Ambapo makampuni kadhaa ambayo yalishiriki katika maonyesho hayo na kushindanishwa katika ubora wa bidhaa pamoja na vifungashio Asas dairies waliibuka washindi.
Katika maonyesho hayo Makampuni na wajasiriamali kadhaa wanaojihusisha na usindikaji wa bidhaa za maziwa walishindanisha bidhaa zao . kwa upande wa makampuni makubwa yaliyoshiriki maonyesho hayo ni  Tan Dairies ya Dar es salaam,Tangafresh ya Tanga,Engiten ya Arusha, Cefa ya Njombe na Asas Dairies ya Iringa. Kwaupande wa vikundi vingine ni  Nronga group ya Kilimanjaro, kalali group ya kilimanjaro Jitume, uvingo group, Agape group,Profet investiment. Victoria Maziwa mara, fukeni mini dairies, vwawa Cooperatives,na  Inuka groupe. Ambapo Asas Dairies Ilishinda  kwa kutwaa gold medal kadhaa pamoja na kuwa mshindi wa jumla wa maonyesho hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari mwakilishi wa kampuni ya Asas dairies kwa nyanda za juu kusini Jimmy Kiwelu kwanza aliwashukuru wananchi wa mkoa wa Ruvuma kwa mwitikio walio uonyesha kwa kujitokeza kwa wingi .
Pia aliongeza kuwa kama kampuni anatoa rai kwa wana Ruvuma kwa ujumla kuendelea kutumia bidhaa za Asas dairies kwani wamepania kufungua sales Depot hapa mkoani Ruvuma na kwamaana hiyo watakuwa na uhakika waupatikanaji wa bidhaa za Asas dairies kwa wingi kabisa.
Akizungumzia ushindi walio upata Mr.Jimmy kiwelu anasema kwaushindi ambao kampuni ya Asas dairies waliopata inadhihirisha ninjinsi gani Asas dairies walivyojikita katika Ubora wa bidhaa na pia vifungashio vya kiwango cha kimataifa.
Aliendelea kusema kuwa kwaushindi huu kampuni imepania kuongeaza uzalishaji na kufika kila kona ya Tanzania na kusisitiza kuwa swala la ubora wabidhaa kwao ndiyo kipaumbele cha kwanza na kutoa shime basi watanzania waendelee kuiamini Asas dairies na wanywe maziwa yaliyo sindikwa na Asas Dairies kwa Afya Bora. Chanzo: Fuad

0 comments:

Post a Comment