Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 30 May 2013

Watu 64 wafa katika mapigano ya kikabila Sudan

                                 21Rajab,1434 Hijiriyah/ May 31,2013 Miyladiyah
 Duru za habari nchini Sudan zinaarifu kuwa, mapigano ya kikabila yaliyotokea katika jimbo la Darfur Kusini yamepelekea watu wasiopungua 64 kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa. Gazeti la Al-Ahram linalochapishwa nchini Sudan limewanukuu viongozi wa jimbo la Darfur Kusini wakithibitisha kujiri mapigano makali kati ya makabila mawili katika jimbo hilo yaliyosababisha wa 64 kuuawa. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mwezi Machi mwaka huu, kulitokea pia mapigano makali kati ya makabila hayo mawili huku chanzo kikitajwa kuwa ni tofauti kuhusiana na ardhi. Migogoro ya kikabila imeshtadi katika siku za hivi karibuni katika jimbo la Darfur. Siku kadhaa zilizopita pia, watu 130 waliuawa baada ya kutokea mapigano ya kikabila huko magharibi mwa jimbo hilo nchini Sudan.

0 comments:

Post a Comment