Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 30 May 2013

Rais wa Kenya azungumzia mishahara ya wabunge

                                  21Rajab,1434 Hijiriyah/ May 31,2013 Miyladiyah
 Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema Tume ya Mishahara na Marupurupu SRC ndiyo iliyopewa jukumu la kikatiba la kuamua mishahara ya maafisa wote wa serikali na kulitaka Bunge liheshimu maamuzi ya tume hiyo. Kiongozi huyo ametoa wito kwa wabunge kushauriana na SRC na kutatua mzozo kuhusu mishahara yao. Rais Kenyatta amesema maafisa wote wa umma na serikali kuu wataendelea kuheshimu mishahara ya SRC. Rais wa Kenya amesema kupitia taarifa kwamba amekasirishwa mno na malumbano ambayo yamekuwa yakiendelea kwa majuma kadhaa kati ya wabunge na tume ya SRC. Taarifa yake inafuatia hatua iliyochukuliwa na wabunge siku ya Jumanne ya kufuta ilani ya SRC iliyopunguza mishahara ya wabunge kutoka shilingi 851, 000 hadi 532, 000. Mwenyekiti wa SRC, Bi. Sarah Serem amesema chombo chochote kitakachoongeza mishahara ya wabunge kitachukuliwa hatua za kisheria kwani tume yake ndiyo yenye mamlaka ya kikatiba ya kuongeza au kupunguza mishahara ya watumishi wa umma na maafisa wa serikali.

0 comments:

Post a Comment