Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 30 May 2013

Polisi ya Uganda yaondoka makao makuu ya Monitor

                                               21Rajab,1434 Hijiriyah/ May 31,2013 Miyladiyah
 Waziri wa Mambo ya Ndani anayeondoka nchini Uganda, Hillary Onek ametoa amri kwa polisi kuondoka mara moja kwenye makao makuu ya shirika la Monitor Publications linalochapisha gazeti la kila siku la Daily Monitor. Onek amesema shirika hilo liko huru kuendesha shughuli zake bila ya kubughudhiwa na yeyote. Duru za habari zinaarifu kuwa, polisi tayari wameondoka kwenye shirika hilo na wafanyakazi wameanza shughuli zao. Itakumbukwa kuwa, polisi walivamia makao makuu ya shirika hilo Mei 20 na kulizingira hadi mapema leo asubuhi kwa madai kwamba gazeti la shirika hilo lilichapisha habari yenye kuhatarisha usalama wa taifa. Kitendo cha polisi kuvamia Monitor Publicationsh kililaaniwa na mashirika mbalimbali ya kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa.

0 comments:

Post a Comment