21Rajab,1434
Hijiriyah/ May 31,2013 Miyladiyah
Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda, ametiwa
mbaroni nchini Norway. Habari kutoka Norway zinasema kuwa, mtu huyo
aliyetiwa mbaroni anatuhumiwa kutenda jinai tofauti wakati wa mauaji ya
kimbari na kwamba, alikuwa akiishi nchini humo kwa kipindi cha miaka 13.
Leo mahakama ya nchi hiyo inatarajiwa kuchukua uamzi kuhusiana na
kadhia hiyo. Wakili wa mtuhumiwa huyo Harald Stabell amesema kuwa, mteja
wake hakuhusika kwa vyovyote na mauaji ya kimbari nchini Rwanda,
yaliyopelekea watu laki nane kuuawa sambamba na kutaka aachiliwe huru.
Televisheni moja nchini Norway imetangaza kuwa, mwaka uliopita mtuhumiwa
huyo alitiwa mbaroni kwa tuhuma hizo na kuachiliwa huru hapo baadaye.
Mauaji ya kimbari nchini Rwanda, yalitokea mwaka 1994 baada ya kuanguka
ndege iliyokuwa imembeba rais wa wakati huo Juvenal Habyarimana karibu
na mji mkuu wa nchi hiyo Kigali.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment