Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Monday, 20 May 2013

Waasi: Tuhuma za Sudan hazijavuruga safari ya Kiir

 
 
Kiongozi wa Harakati ya Ukombozi ya Wananchi wa Sudan ametangaza kuwa, hatua ya kuakhirishwa safari ya Rais Salva Kiir wa nchi hiyo huko Sudan, haihusiani na tuhuma zilizotolewa na Khartoum kwa serikali ya Juba, juu ya kuhusika kwake katika mashambulizi ya waasi ya hivi karibuni huko magharibi mwa Sudan. Hayo yamesemwa na Atim Garang kiongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Ukombozi ya Wananchi wa Sudan huko kusini mwa nchi hiyo na kuongeza kuwa, uakhirishwaji wa safari hiyo ya kiongozi huyo, hauna mafungamano yoyote na tuhuma hizo. Kiongozi huyo amesema kama ninavyomnukuu, "inaonekana viongozi wa Sudan wana wasiwasi na mabadiliko ya Darfur na Kordofan, hivyo wanapanga mkutano wa Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na Omar Hassan Al-Bashir wa Sudan, ufanyike kando ya mkutano ujao wa Umoja wa Afrika, utakaofanyika mjini Addis Ababa Ethiopia." Mwisho wa kunukuu. Wiki iliyopita, balozi wa Sudan Kusini mjini Khartoum Myan Dott, alinukuliwa akisema kuwa, safari ya Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini nchini Sudan iliyokuwa imepangwa kufanyika mwezi huu, imesogezwa mbele hadi katikati ya mwezi ujao wa Juni.

0 comments:

Post a Comment