Duru za habari zimemnukuu afisa mmoja wa usalama nchini Misri akisema
kuwa, watu wanne wametiwa mbaroni kwa tuhuma ya kushambulia msafara wa
Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo. Afisa huyo ambaye ni kiongozi wa
idara ya usalama mjini Cairo amewambia waandishi wa habari kuwa, idadi
ya watu waliotiwa mbaroni kwa kuhusika katika shambulizi hilo
lililotokea katika mji wa Nasr dhidi ya msafara wa Muhammad Ibrahim,
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri, imefikia wanne. Shambulizi hilo
lilitokea katika mtaa wa Mustapha al-Nuhas mjini Nasr, baada ya kuzuka
mapigano katika mtaa huo kati ya watu wenye silaha waliokuwa
wakigombania umiliki wa eneo mjini hapo. Aidha wakati mapigano hayo
yakiendelea, msafara wa waziri huyo wa mambo ya ndani wa Misri na ambaye
anaishi katika mji huo, ulikuwa ukipita na hivyo kushambuliwa. Wiki
kadhaa zilizopita pia, Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hisham Qandil,
alinusurika kifo baada ya mtu mmoja mwenye silaha kuushambulia msafara
wake katika viunga vya mji mkuu Cairo.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment