Wanaharakati nchini Uingereza, wamefanya maandamano mjini London,
wakiwaunga mkono wafungwa wa jela ya Guantanamo. Maandamano ya
wanaharakati hao waliokuwa wamevalia mavazi yanayofanana na yale ya
wafungwa wa jela ya Guantanamo, yalifanyika mbele ya ubalozi wa Marekani
mjini London na kuonyesha mafungamano wao na wafungwa wa jela hiyo. Hii
ni katika hali ambayo, siku ya Ijumaa iliyopita, kundi moja la
wanaharakati wa Marekani waliovalia mavazi kama hayo walikusanyika mbele
ya ikulu ya Marekani White House na kutaka kuachiliwa haraka wafungwa
hao. Karibu wafungwa 130 wa jela hiyo ya kutisha wanaendelea na mgomo
wao wa kula chakula kwa siku 103 sasa, wakilalamikia hali mbaya ya jela
hiyo. Ni vyema kuashiria hapa kuwa, baada ya Rais Barack Obama wa
Marekani kuingia madarakani, aliahidi kuifunga jela hiyo, lakini
hajatekeleza ahadi hiyo.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment