Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 9 May 2013

Upinzani Guinea Conakry waakhirisha maandamano
Kiongozi wa upinzani wa Guinea Conakry ameakhirisha maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika leo ili kuruhusu mazungumzo ya upatanishi wa Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuhitimisha machafuko yaliyozuka kutokana na kucheleweshwa tarehe ya uchaguzi wa Bunge.
Sidiya Toure amesema, wameamua kuakhirisha maandamano yao ili kuruhusu Umoja wa Mataifa kupatanisha na kuyapa fursa mazungumzo. Watu wasiopungua 20 waliuawa wengi wao kwa kulengwa risasi huku zaidi ya wengine 300 wakijeruhiwa katika ghasia na machafuko yaliyotokea kati ya wafuasi wa upinzani, vikosi vya usalama na wanaomuunga mkono Rais Alpha Conde wa Guinea.
Wapinzani wanamtuhumu Conde kuwa ana nia ya kuiba kura na wanataka orodha ya wapiga kura iangaliwe upya, suala ambalo limepingwa na serikali

0 comments:

Post a Comment