Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 9 May 2013

Iran yazindua chombo cha kutegua mabomu baharini




Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Admeli Habibullah Sayyari amezindua chombo cha kutegua mabomu baharini kilichotengenezwa hapa nchini.
Akizungumza Jumatano ya leo, Admeli Sayyari amesema Iran ni kati ya nchi chache duniani zenye uwezo wa kutegua na kuondoa mabomu baharini. Kamanda huyo ameyasema hayo pembizoni mwa mazoezi ya kutegua mabomu baharini yanayofanyika katika eneo la baharini kusini mwa Iran ambapo mfumo huo umezinduliwa. Sayyari amesema Jeshi la Wanamaji la Iran linafuatilia kwa karibu harakati za vikosi vya kigeni katika eneo la Ghuba ya Uajemi ili kuhakikisha kuwa hakuna tishio lolote dhidi ya nchi. Amesema Jamhuri ya Kiislamu imethibitisha kuwa nchi za eneo zinaweza kudhamini usalama wa eneo pasina kuwepo vikosi vya kigeni. Siku ya Jumanne Jeshi la Wanamaji la Iran lilianzisha mazoezi ya kutegua mabomu baharini mashariki mwa Lango Bahari la Hormuz na Ghuba ya Oman. Iran mara kwa mara imezihakikishia nchi za eneo kuwa uwezo wake mkubwa wa kijeshi si tishio kwani lengo lake ni kujihami.

0 comments:

Post a Comment