Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Friday, 10 May 2013

Uingereza nchi yenye makosa mengi ya kidaktariMakosa mengi yamekuwa  yakifanyika wakati wa kufanyika oparesheni kwenye hospitali kadhaa za serikali nchini Uingereza. Taarifa iliyotolewa na Taasisi ya Kitaifa ya Afya na Tiba ya Uingereza imeeleza kuwa, katika kipindi cha miaka minne iliyopita, jumla ya makosa makubwa 762 yalifanywa wakati wa kufanyika upasuaji katika hospitali za serikali nchini humo. Dakta Michael Durkin Afisa wa Usalama wa Wagonjwa katika taasisi hiyo amekiri juu ya kutokea makosa hayo na kusema kuwa, kupatikana makosa zaidi ya 700 katika kipindi cha miaka minne, ni janga kubwa kwa taifa hilo.

0 comments:

Post a Comment