Efrain Rios Montt Rais wa zamani wa Guatemala amehukumiwa adhabu ya
kifungo cha miaka 80 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kutenda jinai
za kivita nchini humo. Mahakama Kuu ya Guatemala jana ilimhukumu
dikteta Montt adhabu hiyo baada ya kumpata na hatia ya kufanya mauaji ya
kizazi, jinai za kivita, ubakaji na mauaji ya halaiki dhidi ya wananchi
wa kabila la Maya nchini humo. Taarifa zinasema kuwa, Jenerali Efrain
Montt mwenye umri wa miaka 86, alifanya mauaji ya halaiki dhidi ya watu
wa kabila hilo wakati alipoongoza mapinduzi ya kijeshi mwaka 1982 nchini
humo. Imeelezwa kuwa, zaidi ya watu 1,700, waliuawa kwenye machafuko
hayo yaliyotokea nchini humo.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment