Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Friday, 10 May 2013

Aopolewa baada ya kukaa chini ya ardhi kwa siku 17Vyombo vya habari vya Bangladesh vimeripoti kuwa, mwanamke mmoja aliyekuwa anafanya kazi kwenye kiwanda cha ushonaji wa nguo nchini humo, ameopolewa kwenye kifusi cha ghorofa akiwa hai baada ya kupita siku 17 tokea litokee tukio hilo. Taarifa zinasema kuwa, mwanamke huyo ameopolewa akiwa chini ya kifusi, wakati zoezi la kufukua na kuondoa viwiliwili bado linaendelea nchini humo. Hadi sasa zaidi ya wahanga elfu  moja wameshaondolewa chini ya kifusi kwenye  jengo hilo lililokuwa na ghorofa nane. Inafaa kuashiria hapa kuwa, jengo la ghorofa nane lililokuwa likitumiwa na kiwanda cha ushonaji wa nguo liliporomoka siku ya tarehe Jumanne ya tarehe 23 Aprili mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment