Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametaka yawepo mashirikiano zaidi kwa nchi
za Kiafrika. Akizungumza mwishoni mwa kikao cha Jukwaa la Kimataifa la
Uchumi mjini Cape Town nchini Afrika Kusini hapo jana, Rais Uhuru
Kenyatta ameongeza kuwa, mashirikiano ya kieneo na uthabiti wa amani, ni
miongoni mwa malengo ya kimsingi ya nchi za Kiafrika yenye shabaha ya
kuelekea kwenye ustawi katika miongo ijayo. Aidha ametaka zifanyike
juhudi za kuwepo soko moja lenye nguvu katika eneo la ukanda wa Afrika
Mashariki. Inafaa kuashiria hapa kuwa, lengo la kufanyika kikao kama
hicho cha kimataifa, ni kuchunguza changamoto za kiuchumi na kijamii
zinazolikabili bara la Afrika na hali kadhalika kupanga mikakati mipya
yenye shabaha ya kuinua na kuiboresha zaidi sekta ya uchumi katika nchi
za Kiafrika.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment