Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 7 May 2013

Somalia yaomba uwekezaji wa kimataifa

Rais Hassan Sheikh Mohamoud wa Somalia ametoa wito wa uwekezaji zaidi katika nchi yake ambayo inajikwamua kutoka katika machafuko ya zaidi ya miongo miwili. Ameswema hayo leo Jumanne katika ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Somalia linalofanyika London, Uingereza. Wawakilishi wa zaidi ya nchi 50 pamoja na taasisi za kimataifa wameshiriki katika kongamano hilo la siku moja ambalo linalenga kusaidia ujenzi mpya wa Somalia baada ya mgogoro wa muda mrefu. Rais Mohamoud amesema kuwa, kadhia ya Somalia ni muhimu kwani ina taathira kieneo na dunia nzima.
Kongamano hilo la wafadhili wa Somalia pia limehudhuriwa na viongozi wa nchi zinazopakana na Somalia akiwemo Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Aidha wawakilishi wa Shirika la Fedha Duniani, Benki ya Dunia, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa nao wamehudhuria mkutano huo.
Wakati huo huo imearifiwa kuwa mkuu wa Shirika la Kijasusi la Qatar ameuawa  katika mripuko wa bomu mjini Mogadishu jana Jumatatu. Kwa mujibu wa gazeti la Ad-Diyar la Lebanon, jasusi huyo mkuu wa Qatar alikuweko Somalia kupanga namna magaidi kutoka Yemen watakavyotumwa Syria baada ya kupewa mafunzo na vikosi maalumu vya Marekani nchini Qatar.
 

0 comments:

Post a Comment