Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 7 May 2013

Mgomo wa wafanyakazi Ulaya wazidi kushika kasi

 Maelfu ya wafanyakazi wa Umoja wa Ulaya, wameendelea na mgomo katika kulalamikia utekelezaji wa mpango wa kubana matumizi katika nchi za jumuiya hiyo. Leo wafanyakazi 3500 wa Baraza la Umoja wa Ulaya wamefanya maandamano mgomo mjini Brussels, Ubeligiji, kulalamikia kupunguzwa mishahara ya wafanyakazi na kuongezwa masaa ya kazi katika nchi za umoja huo. Navyo vyama vya wafanyakazi barani Ulaya vimetangaza kuwa, katika kipindi cha miaka 15 iliyopita, wafanyakazi wa moja huo unaoundwa na nchi wanachama 27, wamepungukiwa na asilimia 60 ya uwezo wa manunuzi, suala ambalo linatokana na siasa za kubana matumizi za serikali za nchi za bara hilo. Kuongezwa miaka ya kustaafu, ni miongoni mwa mambo yananolalamikiwa pia na wafanyakazi wa nchi za Ulaya.

0 comments:

Post a Comment