skip to main |
skip to sidebar
TAMKO LA BAKWATA KUHUSU MLIPUKO WA BOMU JIJINI ARUSHA
TAMKO LA BARAZA KUU LA WAISLAMU WA TANZANIA BAKWATA JUU YA MLIPUKO WA BOMU - ARUSHA
Assalaam alaykum warahmatullahi wabarakaatuh.
Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA, limepokea kwa masikitiko
makubwa tukio la kurushwa bomu Kanisani na kusababisha upotevu wa maisha
na majeraha kwa watu wengi wakati wa sherehe ya uzinduzi wa jengo la
Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Orasiti, Arusha.
Kimsingi hili ni jambo la kusikitisha, kukera na kufadhaisha sana
kutokea hapa nchini. Watanzania kwa miaka mingi, tumezoea hali ya
utulivu na amani na tukio kama hili ni changamoto kwa usalama wa
Watanzania wote nchi nzima Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA
linalaani kitendo hicho cha kikatili na inaviomba vyombo vya dola
kufanya jitihada zote kuhakikisha wahusika wanakamatwa na wanachukuliwa
hatua, kwani msiba huu ni wetu sote, Wakristo na Watanzania wote.
Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania mimi Sheikh Issa Bin
Shaaban Simba Mufti wa Tanzania nawapa pole wafiwa wote katika tukio
hilo na kuwaombea dua majeruhi na Mwenyezi Mungu (SW) awape tahfif na
wapone haraka na kurudi katika shughuli zao za kila siku.
Wabillahi Tawfiiq.
SHEIKH ISSA BIN SHAABAN SIMBA.
MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIA BARA.
0 comments:
Post a Comment