Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 7 May 2013

Robinson: Askari wa UN wawe waangalifu Kongo

Mkuu wa Kamisheni Kuu ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ameonya juu ya athari za uharibifu kwenye operesheni za vikosi vya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Akilihutubia Baraza la Usalama la umoja huo, Mary Robinson amesema kuwa, vikosi vya kimataifa vilivyoko nchini Kongo vinapaswa kufanya operesheni zake kwa uangalifu mkubwa ili kuepusha kujitokeza athari mbaya na maafa nchini humo. Amesisitiza kuwa, iwapo operesheni hizo hazitafanyika kwa njia sahihi, kuna hatari ya kujitokeza maafa makubwa kwa wananchi wa nchi hiyo.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, tarehe 29 Machi 2013 Baraza la Usalama liliafiki kutumwa vikosi vya kimataifa nchini Kongo kwa shabaha ya kukabiliana na makundi ya waasi.
 

0 comments:

Post a Comment