Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 7 May 2013

Iran: Hukumu dhidi ya Wairani itazamwe upya Kenya

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, raia wawili wa Iran waliotiwa mbaroni nchini Kenya na kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha ni wahanga wa iliyopangwa hapo awali. Ramin Mehmanparast ameongeza kuwa, raia hao wa Kiirani waliingia nchini Kenya mwaka jana kihalali wakiwa na viza kwa shabaha ya kuitembelea nchi hiyo, amma walitiwa mbaroni tarehe 19 Juni mwaka jana na kubambikiwa kesi ya ugaidi kutokana na njama maalumu zilizopangwa dhidi yao. Mehmanparast ameeleza kusikitishwa na hukumu hiyo isiyo ya kiadilifu iliyotolewa na mahakama ya Kenya ya kuwafunga kifungo cha maisha. Amesema kuwa hukumu hiyo haikubaliki na ametaka iangaliwe upya.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, uhusiano wa Iran na Kenya iwe katika serikali iliyopita au serikali ya sasa ni mzuri na unaostawi na akaeleza matumaini yake kwamba serikali ya Nairobi italiangalia na kulichunguza  suala hili kwa makini na kwa uhuru mpana zaidi.

0 comments:

Post a Comment