Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 7 May 2013

Mugabe atahadharisha kushadidi machafuko Afrika

Rais Robert Gabriel Mugabe wa Zimbabwe ameonya juu ya njama za nchi za Magharibi za kushadidisha ghasia na machafuko katika nchi za Kiafrika.
Akizungumza mbele ya wakuu wa mashirika ya upelelezi ya nchi za Kiafrika mjini Harare, Rais Mugabe ameongeza kuwa, taasisi za kiusalama za Kiafrika zinapaswa kuwa macho, kwani  nchi za Magharibi ndizo zinazochochea machafuko barani humo kwa minajili ya kupora utajiri na maliasili za barani Afrika. Rais Mugabe ameongeza kuwa, mbinu mpya inayotumiwa na nchi hizo za Magharibi za kupora maliasili za Afrika ni za kuwatumia wanajeshi wa kulinda amani barani Afrika.
Rais wa Zimbabwe amesisitiza kuwa, madola ya kikoloni ya Magharibi yanaanzisha chokochoko na machafuko barani Afrika, kisha yanatumia mwamvuli wa vikosi vya kulinda amani, kwa lengo la kupora maliasili na utajiri wa Afrika.

0 comments:

Post a Comment