Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 7 May 2013

Maguire: Nato inataka kuiangamiza Syria

Mairead Maguire mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1976 amesema kuwa, madola ya kigeni ndio yanayosababisha machafuko na hali ya mchafukoge nchini Syria.
Maquire amesema kuwa, mgogoro wa Syria umesababishwa na uingiliaji wa makundi ya kigeni yanayobeba silaha kwa amri ya madola ya Magharibi na ya Kiarabu. Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ametaka mgogoro wa nchi  hiyo ukomeshwe bila ya uingiliaji wa madola ya kigeni na kusisitiza kuwa, Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zinapaswa kukomesha vita vya Syria na kuwaachia wananchi wa nchi hiyo kuanzisha mchakato wa kutatua mgogoro huo bila ya uingiliaji wa madola ya kigeni.
Mairead Maguire amesema kuwa, vikosi vya Nato vimefanya uharibifu mkubwa katika nchi za Iraq, Libya na Afghanistan na hivi sasa vinataka kufanya uharibifu na maafa mengine nchini Syria.

0 comments:

Post a Comment