Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 28 May 2013

Rais Kikwete atoa pendekezo mgogoro wa DRC
Rais Jakaya Kikwete amependekeza Jumuiya ya Kimataifa ijielekeze kutafuta suluhu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) kwa njia ya mazungumzo badala ya kutegemea ufumbuzi kwa njia ya kijeshi pekee.

Rais Kikwete alitoa pendekezo hilo juzi wakati wa mkutano wa kwanza wa Mchakato wa Kikanda wa Usimamizi wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika DRC na Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGRL).

Pendekezo hilo lilikubaliwa na mkutano huo uliohudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), wakuu wa nchi wanachama wa ICGRL, na viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Mkutano huo unafanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia ambako Rais Kikwete na viongozi wengine wanaohudhuria Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa AU.


0 comments:

Post a Comment