Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 28 May 2013

ZEC: Tutaandikisha wote wenye sifa daftari la wapiga kuraTume  ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), imesema hakuna mwananchi ambaye hatoandikishwa katika daftari la wapiga kura wa kudumu kama atakuwa amekamilisha sifa na vigezo kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya visiwani humo.

Hayo yalisemwa na Kamishna wa Tume hiyo, Nassor Khamis Mohamed, alipokuwa akijibu hoja za wadau mbalimbali waliokuwa wakijadili mpango kazi wa miaka mitano wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.

Alisema ZEC lengo lake kubwa ni kuona kila mwananchi mwenye sifa anapata nafasi ya kusajiliwa katika daftari la kudumu la wapiga kura, kwa vile haki ya kuchagua na kuchaguliwa ni ya Kikatiba na inamhusu kila mwananchi wa Zanzibar.

Hata hivyo aliwataka viongozi wa vyama vya siasa na wadau kusaidia kutoa elimu ya uraia ili wananchi waweze kufahamu haki zao na taratibu za kisheria kushiriki uchaguzi mkuu wa Zanzibar.


0 comments:

Post a Comment