Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 23 May 2013

Polisi lamshikilia askari wake kwa kutorosha mtuhumiwa

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linamshikilia Ofisa wa jeshi hilo, Inspekta Isaack Manoni kwa tuhuma za kumtorosha mtuhumiwa wa usafirishaji magunia ya bangi,Koplo Edward, ambaye alikuwa dereva wa gari la Polisi lenye magunia hayo, namba za usajili T. 2025 Toyota Land Cruser.

Akizungumzia tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema katika sakata la usafishaji bangi kwenda mpaka wa Holili, watuhumiwa walikuwa wawili na askari mwenye namba G.2434 PC George, ambao wote wamefukuzwa kazi mara moja.

Alisema watuhumiwa hao walipelekwa kwenye nyumba zao, kwa upekuzi ndipo walipokuwa nyumbani kwa mtuhumiwa huyo alikimbia na kutokomea kusikojulikana.

“Wakati wakiwa katika nyumba ya mtuhumiwa huyu, kulikuwa na askari saba, akiwamo Inspekta Isaack ambaye alikuwa kiongozi, hivyo baada ya tukio lazima tumshikilie huyu kwa uzembe kazini,” alisema.

Alisema baada ya jeshi hilo kumaliza mahojiano na ofisa huyo, hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.

Aidha, mtuhumiwa mmoja PC. George, mwenye namba za usajili G.2434 amefikishwa Mahakamani, Mkoani Kilimanjaro.

Awali watuhumiwa hao walikamatwa Mei 18 mwaka huu, majira ya saa 5 usiku, huko Himo na askari Polisi wa Kilimanjaro, wakiwa na gari la Polisi lenye namba za usajili T.2025 Toyota landa Cruser lililokuwa likiendeshwa na Koplo Edward, huku likiwa na magunia 18 ya bangi,yakipelekwa Holili mpakani Kenya.

0 comments:

Post a Comment