Wasomi na shakhsia mbalimbali wa kisiasa na kidiplomasia wa kieneo na
kimataifa, wamefanya sherehe ya kumuenzi mwandishi na mwanamapambano
mkubwa wa Tunisia aliyekuwa akipambana na utawala haramu wa Kizayuni
Dkt. Hussein at-Triki. Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi, wanasiasa
na wanadiplomasia mbalimbali kutoka Iran, Lebanon, Algeria, Venezuela
na nchi nyengine za dunia. Katika sherehe hizo Katibu Mkuu wa Chama cha
al Ghad kinachounga mkono mapambano ya muqawama dhidi ya wavamizi wa
Kizayuni nchini humo Omar al-Shahid, alizungumzia sifa ya kipekee
aliyokuwa nayo Hussein at Turiki katika kupambana na dhuluma na kusema
kwamba, msomi huyo alikuwa nguzo muhimu katika mapambano na Wazayuni.
Mwezi Mei mwaka jana at Triki maarufu kwa jina la Sheikh wa
wanamapambano wa Tunisia, aligongwa na gari wakati akitoka kusali katika
msikiti uliokuwa karibu na nyumba yake na kufariki dunia akiwa
hospitalini. Wakati huo huo kiongozi wa kundi la Kisalafi linalojulikana
kwa jina la Ansaru al-Sharia, Seifu al-Din bin Huseein amesema kuwa,
Tunisia inakaribia kuingia katika vita vya ndani. Seifu al-Din
anayetafutwa na vyombo vya usalama vya nchi hiyo, ameitaja hatua ya
serikali ya Tunis ya kuanzisha oparesheni dhidi ya ugaidi kuwa, ni
kuanzisha vita vya ndani nchini humo.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment