Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 14 May 2013

Kesi ya binamu yake Gaddafi yaakhirishwa

                           


Mahakama ya jinai ya mjini Cairo, Misri imeakhirisha kusikiliza kesi ya binamu yake Kanali Muammar Gaddafi wa Libya, Ahmed Gaddafi al Dam. Habari zinasema kuwa, mahakama hiyo inayoongozwa na jaji Mustapha Hassan Abdullah, imeamua kuakhirisha kusikiliza kesi ya al Dam, aliyekuwa mratibu wa mahusiano kati ya Misri na Libya, kufuatia ombi la mawakili wake waliotaka hukumu hiyo iakhirishwe hadi kesho tarehe 15 Mei. Mnamo tarehe 9 mwezi Machi mwaka huu, askari wa usalama nchini Misri walifanya operesheni yao katika eneo la Zamalek katikati ya mji mkuu Cairo anakoishi binamu huyo wa Gaddafi, suala ambalo lilizusha mapigano kati ya polisi wa Misri na walinzi wa Ahmed Gaddafi. Kufuati kitendo hicho, Polisi ya Kimataifa Interpol ilitoa amri ya kutiwa mbaroni mtuhumiwa huyo. Tarehe 19 mwezi huo huo Ahmed Gaddafi al Dam aliwafyatulia risasi Polisi wa Kimataifa wa Interpol pamoja na polisi wa Misri katika wakati walipojaribu kumtia mbaroni binamu huyo wa Kanali Muammar Gaddafi na kumjeruhi afisa mmoja. Idara ya mahakama nchini Misri imepinga kumkabidhi Ahmed Gaddaf al Dam kwa serikali ya Libya na imetangaza kumshitaki katika mahakama zake huku ikiwa tayari imeshamsaili.

0 comments:

Post a Comment