Maelfu ya watu wameripotiwa kuyakimbia makazi yao katika jimbo la
Kordofan Kaskazini huko Sudan kufuatia mashambulio ya hivi karibuni ya
waasi katika jimbo hilo.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kamati ya Misaada ya
Kibinaadamu kwa wakimbizi wa Sudan. Suleiman Abdur- Rahman amesema
kuwa, mashambulio ya waasi katika jimbo la Kordofan Kaskazini
yamesababisha watu thelathini na mbili elfu kuwa wakimbizi.
Taarifa
zaidi zinasema kuwa, tayari serikali ya Sudan imeanzisha operesheni za
upelekaji misaada na mahitaji ya lazima kwa wakimbizi hao walioyakimbia
makazi yao baada ya kushadidi mashambulio ya waasi wanaojulikana kwa
jina la Harakati ya Kimapinduzi. Wakati huo huo,
Msemaji wa Umoja wa
Mataifa amesema kuwa, asasi za utoaji misaada zinazofungamana na umoja
huo zimeanzisha operesheni za kupeleka misaada ya kibinaadamu katika
baadhi ya maeneo ya Jimbo la Kordofan Kusini ambako nako hali ya
kibinaadamu inaripotiwa kuwa mbaya.
Martin Nersiky, Msemaji wa Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, ofisi ya uratibu wa misaada ya
kibinaadamu imesema kuwa, wafanyakazi wa ofisi hiyo wameshapatiwa suhula
kwa ajili ya kuwahudumia watu elfu 40 ambao hivi karibuni waliyakimbia
makazi yao katika jimbo hilo.
0 comments:
Post a Comment