Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday, 11 May 2013

‘Israel ni utawala wa kibaguzi’

                                         02,RAJAB,1434 Hijiriyah/ May 12,2013 Miyladiyah

Muungano wa Palestina Huru nchini Afrika Kusini umeitaja Israel kuwa ni utawala wa Kibaguzi. Taarifa ya muungano huo imelaani vikali muamala na hatua zisizo za kisheria na zinazokinzana na ubinaadamu za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina na kusisitiza kwamba, utawala huo hauna tofauti yoyote na utawala wa zamani wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Muungano wa Palestina Huru umesisitiza kwamba, hatua za kuyayahudisha maeneo ya Wapalestina pamoja hatua za Israel za kuwapokonya Wapalestina haki zao za kimsingi hazina maana nyingine ghairi ya ubaguzi.
Muungano huo umelaani pia hujuma na jinai za kila leo za Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina na kusisitiza kwamba, Wazayuni hawatafanikiwa katika mipango yao ya kuubadilisha mji mtakatifu wa Quds na kuufanya kuwa ni wa Kiyahudi; kwani mji huo mtakatifu ni mali ya Wapalestina. Muungano wa Palestina Huru nchini Afrika Kusini umetahadharisha pia kuhusiana na njama za Wazayuni dhidi ya msikiti mtakatifu wa al-Aqswa.

0 comments:

Post a Comment