Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 14 May 2013

Israel yakiri kumuua Kamanda Mughniya wa Hizbullah




Balozi wa zamani wa utawala wa Kizayuni wa Israel nchini Ujerumani amekiri kwamba Shirika la Kijasusi la Israel MOSSAD ndilo lililopanga na kutekeleza njama za kumuua Emad Mughniya kamanda wa Hizbullah Februari mwaka 2008 mjini Damascus, Syria.
Avi Primor ameyaeleza hayo kwenye mahojiano na kanali moja ya televisheni nchini Ujerumani na kusisitiza kwamba, utawala wa Israel ndio uliotekeleza shambulio la kumuua kigaidi kamanda Mughniya. Hayo yanajiri katika hali  ambayo, utawala wa Kizayuni wa Israel daima umekuwa ukikanusha kumuua Mughniya au kuhusika katika kupanga njama za kutekeleza shambulio hilo la kigaidi.
Waziri Mkuu wa utawala huo ghasibu Benjamin Netanyahu amekuwa akiwataka viongozi wa utawala huo wasizungumze na vyombo vya habari vya Israel  kuhusiana na suala hilo.


0 comments:

Post a Comment