Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 14 May 2013

Bunge la Misri lataka Balozi wa Israel atimuliwe




Bunge la Misri limeitaka serikali ya nchi hiyo kumtimua balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel mjini Cairo.
Ahmad Fahmi Spika wa Bunge la Misri amelaani shambulio la walowezi wa Kizayuni dhidi ya Masjidul Aqswa na kusisitiza kuwa, hatua hiyo ya Wazayuni ya kushambulia Masjidul Aqswa ni kosa kubwa la kihistoria dhidi ya Waislamu na wananchi wa Palestina. Aidha wabunge wa Misri wamezitaka nchi za Kiislamu na Kiarabu kushikamana kwa minajili ya kukomesha uchokozi wa utawala huo ambao hauheshimu hata kidogo na sheria za kimataifa. Wabunge hao wameitaka serikali ya Misri ikate uhusiano wake wa kisiasa na kiuchumi na utawala ghasibu wa Israel.
Hivi karibuni Ahmad Muhammad al Jarwan Spika wa Bunge la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu alilaani mashambulizo hayo ya Wazayuni wenye misimamo ya kufurutu mipaka na kuutaka Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu'Arab League', Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu 'OIC' kuchukua maamuzi ya haraka yenye shabaha ya kunusuru Masjidul Aqswa.


0 comments:

Post a Comment