Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 14 May 2013

Ban ataka mapambano dhidi ya magendo ya binadamu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka zifanyike juhudi zaidi kwa shabaha ya kupambana na magendo ya binadamu ulimwenguni.
Ban Ki moon amesema kuwa, kuna udharura wa kuwepo ushirikiano kati ya nchi, asasi na taasisi zote ulimwenguni kwa shabaha ya kukabiliana na vitendo hivyo hatari kwa amani na usalama wa dunia. Amesema kuwa, magendo ya binadamu huharibu uchumi wa mataifa, kwani mapato ya mabilioni ya dola yanayotokana na biashara hiyo haramu, hutumiwa katika muamala wa kununua na kuuza madawa ya kulevya na jinai nyingine.
Kwa mujibu wa ripoti ya Ofisi ya Kupambana na Jinai na Mihadarati  ya Umoja wa Mataifa  iliyotolewa mwaka 2012, watoto wadogo wanaunda  moja ya tisa ya wahanga wa magendo ya biashara ya binadamu ulimwenguni kote kati ya mwaka 2007 hadi 2010.0 comments:

Post a Comment