Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 14 May 2013

Askari 16 washikiliwa kwa kusaidia biashara ya magendoJeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia askari polisi 16, kwa kosa la kushirikiana na wafanyabiashara za magendo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema hii ni moja kati ya oparesheni ya kusafisha jeshi la polisi na kuwachukulia hatua za kisheria askari wote wanaochafua jeshi hilo.

“Imekuwa ni kawaida askari polisi akifanya vizuri anapewa zawadi pamoja na kuvishwa nishani mbalimbali za utumishi uliotukuka au wa muda mrefu, vivyo hivyo wakifanya vibaya ni lazima wapewe adhabu ama kuchukuliwa sheria kali kama wananchi wengine,” alisema Kova.

Alisema kuwa wafanyabiashara za magendo wamekuwa wakitumia bandari bubu zilizopo katika fukwe za bahari ya Hindi kuanzia Kawe hadi Bagamoyo.
 

0 comments:

Post a Comment